Ommy Dimpoz Afunguka Sababu ya Kumpiga Chini Mubenga. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz Afunguka Sababu ya Kumpiga Chini Mubenga.

Imetimia wiki kama ya tatu tangu kuachiwa ngoma ya Ommy Dimpoz iliyomshirikisha Alikiba ngoma iliyokwenda kwa jina la kajiandae.

Ommy Dimpoz anafunguka sababu za yeye kuachana na aliekuwa meneja wake Mubenga baada ya kudumu nae kwa muda mrefu tokea Nai Nai.

"Watu mnavyoishi katika kazi kunakuwa kuna kiasi fulani cha pesa mnalipana,sasa mimi najua asilimia kubwa wanazolipwa ma-meneja,sasa yeye alikuwa anachukua kiasi kikubwa zaidi.sasa mimi siwezi kuwa nafanya kazi wakati najua kabisa mtu anapiga pesa zaidi inakuwa haina maana bora nifanye tu mishe zangu,hiyo ndio sababu ya kupigana chini na Mubenga" alisema hayo mmiliki wa lebo ya PKP.
Ommy Dimpoz akiwa na Mubenga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.