Nikki wa Pili: 'MTV EMA Kukosea Tuzo ya Alikiba na Kumpa Wizkid ni Kokosa Umakini' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nikki wa Pili: 'MTV EMA Kukosea Tuzo ya Alikiba na Kumpa Wizkid ni Kokosa Umakini'

Nikki wa Pili amesema kosa lililofanywa na MTV EMA, kumtangaza mshindi wa Best Africa Act Wizkid na kisha kuja kumpa Alikiba aliyepata kura nyingi, ni la kibinadamu na kwamba wanapaswa kuwa makini tu.

“Mi naona walikosa umakini, lakini kukosea ni kitu cha kawaida, as long as waligundua wamekosea na wakafanya kitu sahihi sio kama kuna tatizo,” Nikki alimwambia mtangazaji wa kipindi cha The Vibe cha Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny.

Nikki amedai kuwa kosa walilolifanya limeonesha kuwa wao ambao wanatazamiwa kuwa na umakini wa hali ya juu nao hukosea.

Kurudishwa kwa tuzo hiyo kwa Alikiba kulipokelewa kwa furaha kubwa japo mambo yaligeuka kuwa mabaya baada ya watu kuanza kumtukana Wizkid. Hali hiyo ilimlazimu Alikiba kuwaomba watu wasiendelee kufanya hivyo na kudai kuwa mashabiki wake hawawezi kufanya hivyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.