Ngoma Mpya ya Diamond Platnumz na Ne-Yo 'Marry Me' Kupigwa Kwenye Radio/TV Marekani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ngoma Mpya ya Diamond Platnumz na Ne-Yo 'Marry Me' Kupigwa Kwenye Radio/TV Marekani.

Diamond Platnumz amedai wimbo wake mpya ambao haujatoka ‘Marry You’ aliomshirikisha Ne-Yo utachezwa mpaka kwenye vituo vya redio na runinga nchini Marekani.

Hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Salome’ amesema kuwa nyimbo nyingi za wasanii wa Afrika walizowashirikisha wasanii wa Marekani zimekuwa hazichezwi nchini humo.

“Namshukuru Mungu Ne-Yo kanitunuku ni kama bahati wimbo wangu uchezwe mpaka Marekani lakini kwa wasanii wengine wanakataaga,” amekiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.

Tayari video ya wimbo huo imeshafanyika tangu mwezi Septemba mwaka huu huko jijini Los Angeles, Marekani lakini bado haijajulikana muda wa kuachiwa rasmi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.