Mwanamuziki Jaguar Apewa Ubalozi wa Maji. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwanamuziki Jaguar Apewa Ubalozi wa Maji.

Nyota ya muziki wa Kenya, Charles Njagua (Jaguar), imezidi kung’aa baada ya kuzidi kujiongezea wigo mpana wa kuaminika mara baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa maji nchini humo.

Naibu Rais nchini humo, William Ruto pamoja na Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eugene Wamalwa, walimkabidhi tuzo ya ubalozi msanii huyo juzi mjini Nairobi, kwenye ukumbi wa KICC.

Licha ya kuwa balozi wa maji, msanii huyo pia ni balozi wa kupinga dawa za kulevya kupitia shirika la NACADA.

“Ninajisikia kuwa na furaha kubwa kwa Waziri wa Maji kunichagua kuwa balozi katika idara yake, ninaamini nitakuwa balozi wa kweli,” aliandika Jaguar.


Tiffah wa Diamond Akiwa na Gari Yake Aina Ya Bentley. Mtazame Hapa Chini

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.