Mwana FA: Sioni Faida ya Kudandia Muziki Kama Singeli Wakati Naamini Aina ya Muziki Naoufanya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwana FA: Sioni Faida ya Kudandia Muziki Kama Singeli Wakati Naamini Aina ya Muziki Naoufanya.

Rapa Mkongwe Hamis ‘Mwana FA’ Mwin’juma, amefunguka na kusema kuwa anaamini aina ya muziki anaoufanya haoni sababu ya kudandia dandia aina ya miziki inayo ‘Trend’ kwa sasa ikiwemo Singeli.

Akiongea kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm jana, FA amedai hana mamlaka ya kumkataza msanii yeyote kufanya aina ya muziki anayoitaka lakini kwa yeye hatoweza kufanya Singeli. “Kama mtu ameamua kurap juu ya mdundo wa Singeli mi ni nani hadi nimkataze? Kulikuwa na kipindi kila anayerap anataka kuimba, sio mbaya kwenda na Trend, mimi sifikirii kufanya Singeli nauamini sana mziki wangu” Alisema FA.

Katika hatua nyingine rapa huyo amedai wimbo wake mpya wa ‘Dume Suruali’ ni muendelezo wa ‘Bado nipo nipo’ kwani yule bachela asiyetaka kuoa ameoa lakini hataki kuonga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.