Man Fongo Kufunga Ndoa Muda Wowote ‘Mungu Ameagiza’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man Fongo Kufunga Ndoa Muda Wowote ‘Mungu Ameagiza’

Msanii wa muziki wa Singeli Man Fongo amesema yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaamini msanii wa muziki akioa lazima apotee kimuziki lakini hana jinsi ataoa tu kwa kuwa ni agizo la mwenyezi Mungu.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Hainaga Ushemeji’ amesema yeye atafunga ndoa muda wowote kwa kuwa ana mchumba ambaye amedumu naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu.


“Wapo wasanii kibao wameoa halafu wanapotea katika muziki ila kwa mimi Man Fongo na plan ya kuoa kwa sababu mimi watu wangu wa uswahilini,” alisema Man Fongo. “Watu wangu wa uswahilini ndo wamenibeba mpaka wakati huu watu wananielewa, kwa hiyo Man Fongo kuoa lazima nioe kwa sababu Mungu ameleta uharatibu huu ili tuufuate,” Shilole Abadili Jina na Kujiita Shishitrump, Tazama hapa chini akifunguka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.