Lionel Messi Aifungia Barcelona Bao la 500. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lionel Messi Aifungia Barcelona Bao la 500.

Lionel Messi wa Barcelona baada ya kufunga bao lake la 500 siku ya Jumapili.

Klabu ya Barcelona inasheherekea tukio jingine la kihistoria baada ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kuifungia klabu yake bao lake la 500 siku ya Jumapili.

Messi mwenye umri wa miaka 29 aliifungia Barcelona bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.

Messi sasa ameifungia Barca mabao 500 katika mechi 592,ikiwemo mechi za kirafiki huku mechi 469 zikiwa rasmi.

Messi sasa amemshinda aliyekuwa na mabao mengi Paulino Alcantara ambaye aliichezea Barcelona katika vipindi viwili vya kati ya 1912 na 1927.

Mnamo mwezi Aprili,mshambuliaji huyo alifunga bao la 500,ikiwemo mechi za kimataifa,wakati Barcelona iliposhindwa 2-1 na Valencia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.