Lampard Ametangaza Kuondoka Katika Klabu ya New York City ya MLS - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lampard Ametangaza Kuondoka Katika Klabu ya New York City ya MLS

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Chelsea, Frank Lampard ametangaza kuwa anataraji kuondoka katika klabu ya New York City ya MLS ambayo ameitumikia kwa miaka miwili.

Lampard mwenye umri wa miaka,38, ambaye mkataba wake klabuni hapo unamalizika mwishoni mwa mwaka huu, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa muda wake wa kuwepo katika timu hiyo sasa umefika kikomo. Kiungo huyo amewashukuru watu wote walioonesha ushirikiano kwake kwa miaka miwili aliyokuwepo kunako timu hiyo ambapo amefunga magoli 15 kwenye 31 alizocheza. Lampard amesema kuwa hivi karibuni atatangaza ukurasa wake mpya wa maisha yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.