Joh Makini Kumrudisha Lord Eyes Kwenye Game. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Joh Makini Kumrudisha Lord Eyes Kwenye Game.

Rapa mkali kutoka katika kundi la WEUSI Joh Makini amefunguka na kusema kuwa huenda kazi mpya itakayo mrudisha Lord Eyes katika game amefanya naye yeye.

Joh amedai kuwa watu wanatakiwa kuelewa kwamba Lord Eyes ni familia ya WEUSI hivyo hajatengwa kama ambavyo watu wamekuwa wakisema.
Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Joh Makini amesema kuwa siku za karibuni walikuwa studio wakitengeneza kazi ya Lord Eyes mpya ambayo ndiyo anatarajia kuitoa siku za karibuni na kudai kuwa kitendo cha Lord Eyes kuonekana akifanya show zake mwenyewe ni sawa kwani hata yeye huwa anafanya kazi zake nyingine kama Solo Artist.

"Unajua watu wanakuwa wanaongea mambo wasiyojajua lakini si vibaya wacha waongee maana muda mwingine usipoongelewa mtu ni kama unakuwa haupo vile, hili suala la Weusi na Lord Eyes kiukweli mimi mwenyewe 'Iam tired' kwa kweli, Lord Eyes 'still ni part of the family' anaendelea kufanya sollo mimi mwenyewe nafanya sollo Joh Makini kama Joh Makini, Nikki as Nikki, G Nako, Bonta kama Sollo mbona mimi siulizwi kama sollo napiga michongo yangu na mimi nimetengwa? Sijatengwa . Nafikiri moja kati ya ngoma za Lord Eyes anazotarajia kutoa sasa tulikuwa wote studio tukitengeneza pamoja na yeye, kwa hiyo watu wanaongea vitu ambavyo hawavijui" alisema Joh Makini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.