Idris Sultan Adai Mwigizaji Lulu Ni Msichana 'Wife Material' Ila Wao ni Washkaji Tu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Idris Sultan Adai Mwigizaji Lulu Ni Msichana 'Wife Material' Ila Wao ni Washkaji Tu.

Mchekeshaji na mshindi wa Big Brother 2014 Idris Sultan amedai katika tasnia ya filamu, mrembo Elizabeth Michael ‘Lulu’ ndiye msichana mwenye sifa ya kumuoa.

Idris ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Wema Sepetu na baadae kuachana, ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM kuwa Lulu ndiye msichana ambaye anahisi ametulia.

“Mimi naona Elizabeth Michael ametulia sana,” alisema Idris. “Ni staa ambaye namuona yuko vizuri, amesimama, mwenye vigezo vya mwanamke ambaye ametulia, anajiheshimu na vitu kama hivyo.”

Aliongeza,”Lakini mwisho wa siku sisi ni marafiki, yaani unaweza ukanikuta hapo na Lulu yeye amevaa kibikini chake na mimi nimevaa kiboksa changu lakini niwashkaji tu,”

Idris ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, alifunguka hayo baada ya kuulizwa ni mrembo gani bongomovie ambaye anamtamani kutoka naye kimapenzi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.