Hamisa Mobetto Azungumza Haya Mapya Kuhusu Uhusiano wa Kimapenzi na Diamond Platnumz. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hamisa Mobetto Azungumza Haya Mapya Kuhusu Uhusiano wa Kimapenzi na Diamond Platnumz.

Mrembo na Queen wa Video za Bongo Flava, Hamisa Mobeto, amekanusha tetesi zinazoenea mitandaoni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Platnumz.

Kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm juzi Jumamosi, Hamisa amedai kuwa anamfahamu mpenzi wa Msanii huyo Zari kwa kuwa ni Mzazi mwenza wa Platnumz. “Unajua huwezi kusema mi na Zari tuko sawa au hatupo sawa kwa sababu hatujawahi kuwa marafiki na mi nimemjua kwa sababu ‘Kazaa’ na Bosi wangu (Diamond Platnumz). The Only thing nmewahi kumuona Zari kwenye 40 ya Tiffah, We are not Friends We are not enemies, Diamond ni Bosi wangu aliwahi niajiri mimi kuandaa Birthday ya Mama yake.” Alisema.

Katika Hatua nyingine Hamisi alilazimika kufunguka kwa Undani ukaribu wake na Familia ya Diamond akiwemo Mama yake kuliko hata Mama Tee, Zari The Bosslady. “Unajua mpaka Mwanamke kuingia kwenye Nyumba ya Mwanamke mwingine, it means Babu na Bibi wameruhusu, mimi siwezi kujua wameongea nini kitu gani, nnacho jua nilipewa kazi na nikadeliver” Hamisa Mobeto.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.