Gambia Yatangaza Kujitoa Kwenye Mahakama ya ICC. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gambia Yatangaza Kujitoa Kwenye Mahakama ya ICC.

Nchi ya Gambia imetangaza nia yake ya kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC).

Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo, Sheriff Bojang amesema mahakama hiyo ipo kwa ajili ya kuwanyanyasa waafrika. “ICC had been used for the persecution of Africans and especially their leaders,” amesema waziri huyo. Naye msemaji wa umoja wa mataifa (UN), Farhan Haq amesema Gambia itaacha kuwa mwanachama wa mahakama hiyo kuanzia mwezi Novemba mwakani. Gambia itakuwa nchi ya tatu ya Afrika kuingia kwenye mchakato wa kujiondoa kwenye mahakama hiyo baada ya Burundi na Afrika Kusini kutangaza hapo mwazo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.