Dogo Janja na Ishu ya Kuoa Akiwa Bado na Umri Mdogo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dogo Janja na Ishu ya Kuoa Akiwa Bado na Umri Mdogo.

Msanii wa muziki wa kurap kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema ni lazima aingie kwenye maisha ya ndoa akiwa na umri mdogo.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amesema kwa sasa hana muda mrefu ataingia kwenye maisha ya ndoa kwani tayari ameshajianda kukabiliana na changamoto za ndoa.

“Hakuna haja yakuogopa, mimi lazima nioe nikiwa na umri mdogo ndo nimepanga hivyo,” alisema. “Kwanza ni jambo ambalo linampendeza mwenyezi Mungu kwa hiyo ukifika wakati wakufunga ndoa nitafanya hivyo,”

Aliongeza, “Mimi naamini maisha ni haya haya, tena usishangae ukioa mambo yakakunyokea zaidi, kwa hiyo mimi nimesema muda ukifika nafunga ndoa,”

Rapa huyo amesema Tunda Man aliyefunga ndoa hivi karibuni amemfanya nayeye afikirie kuoa siku za usoni.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.