Diana Edward Adaiwa Kuikimbia Kampuni Iliyomtoa Baada tu Yakushinda Taji la Miss Tanzania 2016. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diana Edward Adaiwa Kuikimbia Kampuni Iliyomtoa Baada tu Yakushinda Taji la Miss Tanzania 2016.

Kampuni ya Filamu ya Timamu Effects, imefunguka na kudai kuwa wao ndio waliomuandaa kwa gharama zao Miss Tanzania 2016, Diana Edward kuanzia ngazi ya Kitongoji cha Ubungo ila amewakimbia baada ya kushinda taji la Mlimbwende wa Tanzania.

Akiongea kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Meneja wa Kampuni hiyo Timoth Conrad na Meneja Vipaji Mama Ashura, wamesema mrembo huyo aliingia Timamu akiwa hana wazo la Urembo na wao ndio waliomshauri na ‘kumpika’ katika urembo. “Alikuja kama Muigizaji na Mtangazaji ila sisi tukagundua anaweza kuwa Miss tukaanza kumjenga, tukamuandaa akashinda Ubungo, Kinondoni ila baada ya kushinda taji la Tanzania nzima hatukumbuki, mimi ninachomshauri tu akumbuke alipotoka hatuna haja na zawadi ila heshima ya alipotokea” Alisema Mama Ashura.

Katika hatua nyingine uongozi wa kampuni hiyo umedai unazo nyaraka zote za mkataba aliyosaini Mrembo huyo na Timamu lakini haijaamua bado ‘kumburuta’ Mahakamani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.