Diamond Platnumz Afungukia Wanaotafuta Kiki Kupitia Yeye. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz Afungukia Wanaotafuta Kiki Kupitia Yeye.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wanaojua utamu wa kazi ya mziki wa bongo flava na faida aliyoipata tangu aingie katika tasnia hiyo iliyompa heshima kubwa hasa hapa bongo.

Leo mshale ya mchana kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Diamond amewachana wasanii wanaojaribu kutafuta kiki kupitia jina lake na sio kwa mambo mengine yenye faida zaidi kwenye kazi.

"Mimi nadhani watu wafanye kile ambacho wanaamini ili kufanikisha malengo yao bila kupitia mgongo wa mtu na kuendelea kwenye maendeleo yao tu, mi bora mtu aniambie ili nijue namsaidia nini tofauti ya kutumia jina langu kwenye mambo yake na hili lipo sana kwa baadhi ya wasanii wenzangu ,akijihisi tu anaanza kupotea kwenye game anatumia jina la mtu maarufu kama mimi." alisema Simba wa bongo.

Unakumbuka lile fukuto la Diamond na Ommy dimpoz kuombana msamaha alafu wakapotezeana hasa Bongoswaggz inakupa majibu aliyotoa Diamond baada ya kuulizwa kuhusu Mr Kajiandae.
"Unajua mimi ni mtu ambae naangalia sana maisha yangu na huwa sipendi kuangushwa na mtu, Ommy alipogundua amenikosea alishidwa kunifuata na kuanza kunitumia watu ila 'maneno ya mtoto kumuambia mtoto tunasema wanacheza' na ukiona 'mtoto anamwambia mkubwa tunasema mtoto anakuwa'" alimaliza hivyo Diamond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.