Diamond: Nimefanya Nyimbo 2 na Rich Mavoko. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond: Nimefanya Nyimbo 2 na Rich Mavoko.

Bet Sasa
Mkali wa wimbo ‘Salome’ na mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya wa Rich Mavoko.

Diamond amesema Rich Mavoko ana nyimbo nyingi ndani huku akidai kuna wimbo unaitwa ‘Sijaona’ ambao WCB nzima imekubali lakini yeye anasea bado anaandaa kali zaidi.

“Mimi mwenyewe nimefanya nyimbo nafikiri mbili na Richard na muda wowote zinaweza kutoka,” Diamond alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Sema Richard ni mtu fulani ambaye anajipanga hivyo kipindi hiki anajipanga akianza kufumuka na mabomu yake ni hatari, maana anajipanga kila wimbo akirekodi anakwambia hii bado, akirekodi nyingine tena anakwambia hii bado yaani naweza kusema Richard ni msanii ambaye ana nyimbo nyingi sana kali,”

Aliongeza, “Kuna wimbo pale unaitwa ‘Sijaona’ WCB nzima wanaikubali lakini yeye anakwambia hii bado, ila akisema hivyo akileta ngoma nyingine inakuwa kali zaidi. Kwa hiyo ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu kamjalia kipaji na mwenyewe anakuaga hana papara”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri kitaifa na kimataifa na wimbo ‘Imebaki Story’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.