Bunduki 11 Zakamatwa Kwa Mbunge. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bunduki 11 Zakamatwa Kwa Mbunge.

Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na kukamata watu wanne zaidi.

Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti hili kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa mbunge (jina limehifadhiwa) ambaye bado anasakwa na kikosi kazi hicho.

Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.

Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.

-mwananchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.