Alikiba: Ngoma ya Aje Ilikuja Wakati Sahihi na Kufungua Njia Zaidi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba: Ngoma ya Aje Ilikuja Wakati Sahihi na Kufungua Njia Zaidi.

Ili uipe thamani zaidi ngoma yako ambayo unaamini itapendwa zaidi na kutusua mitaa ya mbele ni kumshirikisha Alikiba msanii anayejua kuzitendea vyema ngoma utakayo mshirikisha.

Alikiba anatamba na kibao cha Aje nyimbo iliyompandisha na kumsogeza kwenye majukwaa na matamasha makubwa zaidi na kuipa thamani kazi yake licha ya kukaa kimya kwa muda mrefu zaidi.

Bongoswaggz inakudropishia faida iliyoletwa na ngoma ya aje na mafanikio yake.

"Ngoma ya aje imekuja na mafanikio yake tofauti na ngoma zingine nilizoziachia na imanipa mkwanja mkubwa zaidi na kunirudisha kwenye line yangu na Sony kunipa mkataba na kuwa msanii wa pili kutoka africa kupewa mkataba huo ,Ngoma ya aje inaheshima yake kiukweli na imenirudisha kileleni zaidi." alisema alikiba.

Baada ya Ommy Dimpoz kumpa nafasi Alikiba kwenye nai nai na kupa nafasi nzuri ngoma hiyo. Mwezi huu tena Ommy Dimpoz amkaribisha Alikiba kwenye ngoma mpya ya 'Kajiandae' ya kwake Dimpoz.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.