Alikiba: Mkataba na Sony Music Hautanifanya Nikae Kimya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba: Mkataba na Sony Music Hautanifanya Nikae Kimya.

Kama ulidhani Alikiba atapotea kwenye ramani ya muziki baada ya kusaini mkataba na kampuni ya Sony Music kama ilivyowahi kuwatokea baadhi ya wasanii wa Afrika – imekula kwako, mwenyewe amefunguka.

Hitmaker huyo wa ‘Aje’ amekiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM, Alhamisi hii kuwa hawezi kukaa kimya zaidi ya miezi mitatu bila ya kuachia nyimbo mpya kitu ambacho amedai kitamfanya awe juu zaidi.

“Nimejiandaa vizuri na pindi unapokuwa unasaini kitu, ina maana kuwa umekubaliana na kila kitu, kwa hiyo mimi pia ninamatakwa yangu na hata wao pia wanamatakwa yao. Kwa hiyo kitu ambacho kipo hapo ni kwenda na agreement. Mimi siwezi kukaa muda zaidi ya miezi tatu bila kutoa ngoma na huo ndio mkataba wangu jinsi unavyosema,” alisema Alikiba.

Muimbaji huyo alifanikiwa kusaini mkataba na kampuni hiyo mwezi Mei mwaka huu na tayari ameshafanikiwa kuachia wimbo mmoja mpaka sasa akiwa chini ya kampuni hiyo.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.