UEFA: Barcelona Yaiua Manchester City ya Kocha Wake wa Zamani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

UEFA: Barcelona Yaiua Manchester City ya Kocha Wake wa Zamani.

Bet Sasa
Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Michuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.
Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu.
Bravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1.

Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.
Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono.

Matokeo ya michezo mingine:

Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven

Paris Saint-Germain 3-0 Basel

Dynamo Kiev 0-2 Benfica

Napoli 2-3 Besiktas

FC Rostov 0-1 Atl├ętico Madrid

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.