Rich Mavoko: Nina Collabo na Diamond na Msanii wa Naijeria. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rich Mavoko: Nina Collabo na Diamond na Msanii wa Naijeria.

Msanii wa WCB, Rich Mavoko amesema kuwa ana collabo amefanya na Diamond na nyingine na msanii wa Nigeria. Amedai kuwa moja kati ya kazi hizo itatoka mwezi ujao.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Mavoko amedai kuwa hivi karibuni mashabiki wake wataelewa ni silaha gani alizonazo kumpeleka next level kama wasanii wengine wa WCB ambao mwaka huu wametajwa kuwania tuzo kibao.

“Wasione tu nimekaa kimya, kuna vitu vingi vizuri, vikubwa ambavyo vinakuja. Tena kuna collabo na Mnaijeria kuna collabo na Diamond. Kwahiyo hatujajua tu ipi kati ya hapo itoke hivi karibuni,” amesema muimbaji huyo.

Kwa upande mwingine Mavoko amesema Ibaki Story umekuwa wimbo mkubwa kwenye career yake kwa kumfikisha kule ambako mwanzo hakuwahi kufika.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.