PSG Wako Tayari Kutoa Euro Milioni 222 Kumnasa Mshambuliaji wa Barcelona Neymar Jr. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

PSG Wako Tayari Kutoa Euro Milioni 222 Kumnasa Mshambuliaji wa Barcelona Neymar Jr.

Paris Saint-Germain wameamua lengo lao kuu ni kumnasa mshambuliaji wa Brcelona Neymar Jr katika kipindi cha dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiazi.

Mabingwa hao wa Ligue 1 wako tayari kuweka mezani dau la euro milioni 222 kwa ajili ya raia huyo wa Brazil kiasi ambacho kitawafanya wampate kutokana na kipengele cha release clause kilichopo kwenye wake na Barcelona (kwa mujibu wa Goal)

Goal wameripoti kwamba, vyanzo vya karibu na mchezji vimethibisha kwamba uhamisho huo ulikaribia kukamilika hadi pale Neymar alipoamua kusaini mkataba mpya na Barcelona.

PSG wanatarajia kurudi tena kwa mchezaji huyo mara baada ya msimu huu kukamilika.

Deal la kumsaijili Neymar litafanikiwa, nyota huyo atashuhudiwa akilipwa mshahara sawa na ule anaolipwa superstar wa Barcelona Lionel Messi.

Mkataba mpya wa Neymar unaomalizika 2021 unathamani ya euro milioni 25 kwa mwaka mbali zaidi na ule wa Messi wenye thamani ya euro milioni 42 kama mshahara wake wa mwaka mzima.

Endapo Neymar atahamia Paris, ataungana na ndugu zake Marquinhos, Lucas Moura pamoja na Thiago Silva kwenye mji kuu wa Ufaransa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.