Meneja wa Alikiba na Yeye Avunja Ukimya, Aelezea ‘Issue’ ya Alikiba Kuzimiwa MIC. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Meneja wa Alikiba na Yeye Avunja Ukimya, Aelezea ‘Issue’ ya Alikiba Kuzimiwa MIC.

Mambo mengi yamezuka baada ya show ya Mombasa rocks festival ambayo mkali wa Marekani, Chris Brown alitumbuiza.

Moja likiwa ni suala la Alikiba kuzimiwa mic alipokuwa akitumbuiza huku akihoji uwepo wa meneja wa Diamond backstage.

Meneja wa Alikiba, Aidan na yeye ameamua kufafanua suala hilo lililoibua vita ya mashabiki wa mafahari hao wawili ambayo ilikuwa imeanza kupotea,
“Sitaki kuingia sana kwenye ishu ya kuzimiwa MIC sijui nini, umeona! Ishu ni kwamba Ali, alianza na Nyimbo ya MacMuga, then AJE ni nyimbo ambayo kila siku huwa anaifungia shoo lakini alii-perfom akijua pale anatakiwa kumaliza kwa zile nyimbo mbili.” Aidan alifunguka kwenye kipindi cha Amplifaya
.
“Lakini yeye wakati anajiandaa kuwaambia watu kwamba he gonna be back on stage, MIC ikakatwa, ndio pale watu wakashindwa kuelewa kwanini Ali ameshuka! Lakini alikuwa anataka kuwaeleza kwamba atarudi, sababu muda ulikuwa haujitoshelezi.”
.
“Lakini hii ishu sio eti alizimiwa MIC sijui na Meneja wa Chris Brown, wenyewe walikuwa na time yao kabisa, wazungu wako proffesional.”

Alimaliza Aidan lakini pia aliligusia la Ali Kiba kuhoji uwepo wa Sallam SK, back stage.
“Alichokizungumza Ali naomba kibaki kama alivyo kizungumza, I think kutokana na tension iliyopo baina ya wasanii wawili au kambi hizi mbili, I don’t think Kama kilikua kitu cha busara kwa Sallam au mtu anayetajwa kuwepo eneo lile kipindi haya mambo yanaendelea. Ingekua ni Mimi labda nimeenda kwenye shoo na msanii wangu hayupo, nisingekuwa NANG’AA NG’AA SANA PALE, Kutokana na kinaweza kutokea kitu chochote kibaya ukahusishwa.”
. “Na ALI hajamtaja kuwa yeye ndio aliyefanya vile, watu wanajaribu kutoelewa! Ila ALI alikuwa anauliza WHAT WAS HE DOING THERE ? yani kibusara tu. Halikuwa jambo la busara kwa yule jamaa kuonekana pale.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.