Mbali na Kufanya Naye Kazi Ndani ya WCB, Rayvanny Amfananisha hivi Diamond Platnumz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbali na Kufanya Naye Kazi Ndani ya WCB, Rayvanny Amfananisha hivi Diamond Platnumz

Msanii kutoka WCB Wasafi Raymond a.k a Rayvanny amefunguka na kusema kuwa vitu vyenye majina mengi siku zote huwa ni hatari sana hivyo hata yeye anashindwa kumuelezea Diamond Platnumz kutokana na moyo wake wa upendo na kujali.

Rayvanny alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kudai kuwa yeye anamkubali sana Diamond Platnumz kwa sababu kwanza ni mtu mwenye moyo wa upendo lakini pia msanii huyo anakumbuka kuna Mungu na pia anakumbuka kuwa kuna kifo ndiyo maana anakuwa anajitoa sana kwa watu na jamii.

” Mungu ana majina mengi sana, Jehova, Mfalme, Mungu wa miungu, Baba wa watu wote halafu pesa pia ina majina mengi sana Pesa, Ankara, Mshiko, Money, Michakato sijui Njere halafu pia Diamond Platnumz ana majina mengi pia sijui Chibu, Dangote, Chibu D, Simba, Toto la Kimanyema so vitu vyenye majina mengi ni hatari sana”.

Rayvanny akaendelea kwa kumuelezea Diamond namna hii: “Kwa hiyo ukiniambia Diamond namuonaje mwenyewe nashindwa kumuelezea sababu kwanza ni mtu mwenye moyo wa ubinadamu, ana moyo wa kukumbuka kama kuna Mungu, kuna kifo ndiyo maana unaweza kumuona kwenye vituo vya watoto yatima anawasaidia, anasaidia vijana wengi ambao wana vipaji anawapa watu fursa, hivyo ni mtu ambaye amefunguliwa na Mungu njia zake ndiyo maana unaweza kuona ana majina mengi na hapo nimekutajia baadhi ya vitu vyenye majina mengi ili uone siri ya vitu vyenye majina mengi vinakuaje”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.