Mambo 5 Muhimu Ambayo Watu Wenye Mafanikio Zaidi Hufanya Kila Siku Mpya Inapoanza (Nawe Unatakiwa Kuyafanya) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mambo 5 Muhimu Ambayo Watu Wenye Mafanikio Zaidi Hufanya Kila Siku Mpya Inapoanza (Nawe Unatakiwa Kuyafanya)

Ulikuwa unajua kuwa jinsi unavyo panga kulitumia lisaa la kwanza la siku yako kunaweza kukupelekea kwenye ushindi au kushindwa ?

Kwamujibu wa uchunguzi, Watu wengi ambao wamefanikiwa kwenye shughuli zao za kibiashara, ujasiriamali na makazini wamekuwa wakifanya mambo matano muhimu kila lisaa la kwanza la asubuhi kwenye siku mpya ambapo kumewapelekea kuwa na siku yenye uzalishaji mkubwa ambapo na wewe unatakiwa kuzifahamu.

Lee Biggins, Muanzilishi na managing director wa CV-Library, anasema: “Wakati inapkuja kwenye uzalishaji na kujipanga kwaajili ya kufanikiwa kwenye siku yako, Ni muhimu kuhakikisha unawekeza nguvuzako na malengo yako kwenye kile unachotaka kukikamilisha.”
Hapa ameshirikisha mambo matano yaumuhimu ambayo kila aliye fanikiwa na anayetaka kuendelea kufanikiwa anayafanya kila ifikapo asubuhi pila kushindwa.
Kufanya mazoezi kabla ya kufanya kazi

Kufanya mazoezi kabla ya kufanya kazi: Amka mapema ufanye mazoezi, Kimbia, GYM, Ruka kamba, Push-up nk kabla ya kufanya kazi ni muhimu. Inasawazisha akili yako na mwili wako kutoka kwenye uchovu kwenye siku nzima ili kusiwe na changamoto.
Richard Brandon anaanza siku yake kwa kuendesha baskeli, Square CEO na co-founderwa mtandao wa Twitter, Jack Dorsey anafanya jog kwa umbali wa mile sita kilasiku.
Pata kifungua kinywa chenye afya.

Pata kifungua kinywa chenye afya: Huwezi kutegemea kuzalisha vyema kama hujaujaza mwili wako ukashiba, Hakikisha asubuhi yako unapata kifungua kinywa chenye kuupa mwili afya kabla ya kuanza kufanya kazi.
Kwa kuanza siku yako vyema, na kuhakikisha unapata nguvu yaku boost kuvu zako, utaona siku yako inakuwa rahisi kwenye kuhakikisha unafikia malengo yako ukiwa na motisha. Watu wengi wenye mafanikio wanauchaguzi mzuri sana kwenye kifungua kinywa chao.
Safisha inbox yako

Safisha inbox yako: Watu wengi wamakuwa na mtazamo wa kulifanya hili ifikapo mchana, Lakini hakikisha unapo fika tu kazini kwako, jishughulishe kwanza na inbox yako. Kama zipo e-mail za kujibu basi zifanyie kazi mapema kabla hujaanza kazi za siku mpya.
Usiwe mtu wa kuweka viporo au kukaa na yaliyo pita kwakuwa yanakusababishia kushindwa kufikia malengo yako mpya.
Amua malengo yako kwenye siku hiyo.

Amua malengo yako kwenye siku hiyo: Pale tu unapo hakikisha umemalizana na inbox yako, Sasa utakuwa umeshajua ni nini unatakiwa kufanya kwa siku hiyo. Hakikisha unapangilia malengo yako kwa siku hiyo na kuhakikisha kuyafikia.
Ukisha pangilia malengo yako ya siku, Itakusaidia kupangilia mudawako na kasi yako ya kufanya kazi ili kuyafikia.
Weka orodha ya vipaumbele vyako

Weka orodha ya vipaumbele vyako: Ukishaamua malengo yako kwenye siku hiyo, Sasa panga list ya vipaumbele. Inawezekana usiweze kukamisha yote kwenye malengo yako kwa siku hiyo ila kunayaumuhimu ya kukamilisha.

Huwezi ukaharibu siku kama ukiwa na orodha ya ni nini unataka kukamilisha kwa siku hiyo, Hii itakusaidia kuwa na kasi ya malengo, itakusaidia uwe mzalishaji mzuri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.