Kanye West Akatisha Show Yake Jukwaani Baada ya Kim Kardashian Kuporwa Mali Zenye Thamani ya $6.7m. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kanye West Akatisha Show Yake Jukwaani Baada ya Kim Kardashian Kuporwa Mali Zenye Thamani ya $6.7m.

Kim Kardashian hatosahau tukio la Jumatatu hii pindi amevamiwa na watu wenye silaha kwenye jumba la kifahari alilokuwa amekodisha jijini Paris Ufaransa.

Majambazi hayo yalikuwa yamevalia sare za polisi. Msemaji wa polisi amedai kuwa mali zilizoibiwa zina thamani ya dola milioni 6.7. Vingi ni vidani vya madini.

Watu hao walimfungia Kim bafuni na kupata muda mzuri wa kukusanya kila walichoweza kukibeba. Tukio hilo limetokea saa nane na nusu usiku. Ripoti zinadai kuwa Kim ameshaondoka Ufaransa kwa kutumia ndege binafsi.

Wakati tukio linatokea, Kanye West, alikuwa jukwaani Meadows Music and Arts Festival New York na alipopewa taarifa aliwaambia mashabiki: I’m sorry, family emergency. I have to stop the show.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.