Je Una Shughuli/Sherehe Lakini Hauna Wazo Lolote Kuifanya Iwe Nzuri Na ya Kipekee Zaidi ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Je Una Shughuli/Sherehe Lakini Hauna Wazo Lolote Kuifanya Iwe Nzuri Na ya Kipekee Zaidi ?

Je umeshawahi kuwaza shughuli/sherehe nzuri zinazovutia na kuwa gumzo sana zinatokeaje ? Hazitokei tu zenyewe HAPANA bali zinaandaliwa kwa ustadi! Ushauri  kutoka kwa waandaji wa mashughuli ndio uti wa mgongo na ndio njia sahihi ya kuanza nayo kabla ya kufanya chochote katika shughuli yako. 
Kila Mwanadamu anakipaji chake kama alivyo msanifu wa nyumba au produza wa mziki ndivyo alivyo Mshauri wa mashughuli katika shughuli yako ili ifane na kupendeza sana kwa kiwango cha juu!
Ulishawahi kufikiri ni rangi gani nzuri ziatapendezesha shughuli yako? 
Au ni nguo gani ukivaa itakupa mwonekano wakuvutia katika shughuli hio ? Je chakula kipendezacho kwa shughuli hio na wapi pakufanyia hio shughuli, jinsi ya kuiandaa, vinywaji gani vitumike iwe mida gani ya siku au mwaka, siku iendeje na muonekano mzima uweje ?

Inachosha sana ukifikiri vyote ivyo! Japo unaweza taka vingi katika shughuli hio na kutokua na uhkika kipi kinafaa na kipi hakifai. Ni wazo la kutisha sana pale unapofikiri je siku yangu ikiharibika, shughuli yangu isipopendeza? Je gauni au suti ntakayovaa isiponipendeza, mwili wangu unaendana na fasheni flani ya mavazi ?, au je rangi hizi zitatupendezesha au tutatisha? Unaweza uliza rafiki au ndugu na asikupe jibu sahihi au usipate mtu kabisa wa kumuuliza na ukafanya shughuli kama bahati nasibu. Washauri wa Mashughuli ndio Suluhisho lako, ndio uwahitajio kwa mda huo. 
Ukikosea hatua hizi za mwanzo za shughuli yoyote ujue shughuli nzima itaharibika. Watumie ili kuondoa hofu yote na vikwazo vyote vya kuharibu siku yako muhimu.

Umevutiwa kujifunza zaidi jinsi yakuandaa shughuli yako ya kipekee ? Wasiliana na mshauri wetu kupitia; 
Simu 0684 315181 
Instagram: Joyheart Events
Facebook: Joyheart Events
E-mail; info.joyheartevents@gmail.com

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.