Hizi ni Tofauti 6 Kati ya Ubongo wa Mwanaume na Mwanamke. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi ni Tofauti 6 Kati ya Ubongo wa Mwanaume na Mwanamke.

1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume hawezi.

2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike
na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.

3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo huo ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso.

4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbalina kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya
jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.

5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.

6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.