Hii Ndio Kauli ya Kim Kardashian Kuhusu Mali Zake na Mitandao ya Kijamii. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hii Ndio Kauli ya Kim Kardashian Kuhusu Mali Zake na Mitandao ya Kijamii.

Kim Kardashian ameapa kutoonesha tena mali zake kwenye mitandao ya kijamii.

Hiyo ni baada ya watu wengi kudai kuwa ndio chanzo cha kuvamiwa Jumatatu hii jijini Paris na kuporwa mali zenye thamani za dola milioni 11 kwa mtutu wa bunduki.

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim amekubali ni kweli alikuwa amezidisha kuringishia mali zake kwenye mitandao hiyo.

Muda mfupi kabla ya kuvamiwa, Kim aliionesha pete ya $4.5m aliyonunuliwa na mume wake Kanye West. Pete hiyo ilikuwa miongoni mwa vitu vilivyoibwa.

TMZ imedai kuwa Kim atakuwa mapumzikoni mwa mwezi mmoja na akirejea atakuwa na mabadiliko makubwa katika jinsi anavyotumia mitandao ya kijamii.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.