Diamond, DJ-D Ommy, Harmonize washinda tuzo za Afrimma 2016 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond, DJ-D Ommy, Harmonize washinda tuzo za Afrimma 2016

Tanzania imeibuka kidedea katika tuzo za Afrimma za mwaka huu zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, Dallas nchini Marekani, kwa kubeba tuzo tatu muhimu.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania imeinyakua tuzo ya aina yake ya mchezea santuli bora barani Afrika, baada ya DJ- D Ommy wa Clouds Fm kupenya na kutajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Diamond Platinumz ameendeleza wimbi la ushindi wa tuzo kwa kutwaa tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki huku Harmonize akiondoka na tuzo ya msanii bora chipukizi.

“Team Tanzania, Mungu ni mwema siku zote,” Harmonize ameandika Instagram baada ya kupata tuzo hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.