Biblia Aliyokuwa Anatumia 2 Pac Imeuzwa Dola $54,000/Milioni 117 za Kitanzania. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Biblia Aliyokuwa Anatumia 2 Pac Imeuzwa Dola $54,000/Milioni 117 za Kitanzania.

Moja ya vitu ambavyo vinatrend kwa sasa ni kuhusu kitabu cha Biblia alichokuwa anatumia 2pac wakati yupo jela kimetajwa kuuzwa kwa $54,000sawa na milioni mia na ushee

Mtandao wa Moments In Time unaojishughulisha na maswala ya autograph unatarajia kuuza Biblia iliyokuwa inatumiwa na 2Pac wakati yupo jela baada ya kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji mwaka 1995, Biblia hiyo ambayo inaonyesha saini ya 2pac pamoja na namba ambayo alikuwa akiitumia huko kifungoni 95A1140.

Februari 15 Mwaka 1995 ndio siku ambayo Tupac alianza kutumikia kifungo chake baada ya kukutwa na mashitaka ya ubakaji, lakini wakati akiwa anatumikia kifungo chake pac aliwahi kuachia Albamu yake ya Me Against The World na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Album yake kushika namba moja katika chati za Billboard 200.


Tangu kutokea kwa kifo cha 2Pac kumekuwa na vitu vingi ambavyo vimekuwa vikiuzwa vya kihistoria vya masanii huyo ambavyo vinafanya baadhi ya mashabiki kutoridhika na maamuzi hayo ambayo yanafanywa, lakini kikubwa zaidi kama pesa zinawafikia walengwa basi hilo litakuwa ni jambo zuri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.