Wema Sepetu Afunguka Maneno Mazito 'Idris ni Katuni' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Afunguka Maneno Mazito 'Idris ni Katuni'

Kweli ya kale hayanuki! Ndivyo unavyoweza kusema kwani licha ya Idris Sultan kuwahi kuwa mpenzi wake na Bongo nzima kuitambua kapo yao, mrembo Wema Sepetu ‘Madam’ amethubutu kusema kuwa zilipendwa wake huyo kuwa ni sawa na katuni.

Wema alifunguka hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wetu ambapo alipoulizwa mtazamo wake kuhusu Idris kutembea na staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga na kama anapatwa na maumivu yoyote ndipo Madam aliponyanyua kinywa chake na kumnanga Idris.

“Mh! Yule hana lolote, Idris ni katuni tu. Siwezi kupoteza muda wangu kumzungumzia mtu kama yeye, kuna vitu vingi vya kuzungumza hilo ni jambo dogo sana kwangu. “Kwanza siwezi kumjadili maana itakuwa ni kama kumpa faida ambayo pengine angepaswa anilipe, please tuongelee mambo ya maana bwana achana na huyo katuni,” alisema Madam.

Alipotafutwa Idris ili aweze kuzungumzia kauli hiyo ya Madam na pengine ana lipi la kujibu, simu yake iliita bila kupokelewa. Jitihada zinaendelea.

Hivi karibuni, zilisambaa picha za Idris na Linah wakiwa kimahaba na kudaiwa kuwa wawili hao ni wapenzi hali ambayo ilisababisha mijadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari kuripoti ‘kapo’ hiyo mpya. Wema na Idris kabla ya kufi kia hatua hiyo, walikuwa wapendanao kwa miezi kadhaa na Wema kufanikiwa kupata ujauzito ambao baadaye ulichoropoka kisha wawili hao kumwagana.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.