Vanessa Mdee Ampigia Hesabu Trey Songz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vanessa Mdee Ampigia Hesabu Trey Songz

Msanii bora wa kike Afrika Mashariki, Vanessa Mdee, ameibuka na kudai kwamba hesabu zake kwa sasa ni kwa mwanamuziki wa Marekani, Trey Songz, ambaye amewahi kushinda tuzo mbalimbali za muziki.

Vanessa kwa sasa yupo katika maandalizi ya kushiriki katika tuzo ya Loeries itakayotolewa nchini Afrika Kusini kutokana na video bora ya wimbo wa ‘Niroge’ kupata umaarufu na kupendwa na wengi.

Vanessa atakutana na Trey Songz katika wimbo wa pamoja wakati wa msimu mpya wa Coke Studio Afrika International Week ambapo ataimba wimbo wa ushirikiano na Patoranking na Trey Songz. Wasanii wengine atakaoshirikiana nao ni Stonebwoy wa Ghana na Yemi Alade wa Nigeria.

“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa tuzo mbalimbali ikiwemo hiyo ninayoshindanishwa nayo nchini Afrika Kusini huwa napata nguvu kufanyakazi kwa karibu na msanii, Trey Songz, kwa kuwa naye ameshinda tuzo mbalimbali,” alieleza Vanessa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.