Upo Tayari Kumwona Tunda Man Akidakia Klabu ya Simba ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Upo Tayari Kumwona Tunda Man Akidakia Klabu ya Simba ?

Baada ya kuiwakilisha bendera ya Bongo fleva katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa dhidi ya Bongo movie katika kuchangia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Tunda Man amesema kwamba anaanza mazoezi rasmi.

Siku ya jumapili ilikuwa ni siku ya shangwe kubwa baada ya Bongo fleva walipokutana na Bongo movie na kuonyesheana mbwembwe katika swala la soka ambapo mchezo huo ulikuwa ni wakuchangia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera, sasa Tunda Man amefunguka kwamba baada ya kufanya vizuri katika mchezo huo, ametangaza kuwa anaanza mazoezi rasmi kuchezea timu ya Simba au Yanga.

Akiongea na Perfect255, Tunda Man amesema kwamba baada ya kufanya vizuri katika mchezo wake, sasa anaanza mazoezi rasmi ili msimu ujao aweze kuchezea timu za ligi kuu sanasana Simba, na akianza mazoezi nao basi ndani ya muda mfupi tu atakuwa ameshaiva, na kuhusiana kumudu kazi yake ya muziki na mpira Tunda man amesema kwake ni rahisi kwani Mic ni usiku na Mpira ni jioni.

“Naanza mazoezi serious soon ili katika msimu ujao nichezee timu kubwa kati ya simba au yanga, ila napenda sana Simba , yeye alikuwa anahisi anakuja kuangalia vichekesho kumbe alikuja kuangalia wachezaji kweli, na nafasi za magoli kipa ni chache sana katika mpira wa Bongo, kwahiyo naanza mazoezi nao najua ikifika muda nitakuwa nishaiva” Alisema Tunda Man.

-Perfect255

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.