Stand United Wanasubiri Barua ya Accacia Watoe Tamko. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Stand United Wanasubiri Barua ya Accacia Watoe Tamko.


Na Halidi Abdulrahman

Uongozi wa Stand United unasubiri barua rasmi ya wadhamini wao ambao ni Kampuni ya Uchimbaji wa Madini, Accacia baada ya kampuni hiyo kutangaza kuvunja mkataba wa udhamini na timu hiyo.

Accacia ilitangaza kuvunja mkataba na timu hiyo mnamo Agosti, 31 mwaka huu kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania huku sababu iliyotajwa kufikia uamuzi huo ikiwa ni migogoro isiyokwisha.

Licha ya taarifa hizo kuzagaa, uongozi wa Stand United kupitia kwa msemaji wake, Deokaji Makomba umesema unasubiri barua rasmi kutoka Accacia ndipo watakaa na wanasheria wao kisha kutoa tamko lao.

"Tunasubiri barua rasmi kutoka Accacia alafu tutaisoma hiyo barua rasmi jinsi inavyoeleza na baada ya hapo sasa na sisi kupitia hata na wanasheria wetu tutaweza kulitolea maamuzi ama tamko kwa hatua hii ambayo wameifikia, mimi nataka niuthibitishie umma kama Stand United Football Club hatuna mgogoro" alisema kwa kirefu msemaji huyo.

Licha ya kukataa kutokuwepo kwa mgogoro ndani ya klabu hiyo, hakuna asiyefahamu kwamba Stand imepasuka pande mbili zinazokinzana na kuvutana huku kila upande ukijiona wenye haki.

Stand United katika michezo yake miwili iliyotangulia haijawahi kushinda kufuatia kutoa sare mfululizo zilizowafanya kushika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo pia itashuka dimbani siku ya Jumamosi kumenyana na Toto Africa kwenye Uwanja wake wa nyumbani huku hatma ya kocha wao Patrick Liewig ikiwa haijulikani baada ya kufukuzwa hotelini kutokana na deni analodaiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.