Sababu ya Wanawake Kupenda Madaktari Wanaume. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sababu ya Wanawake Kupenda Madaktari Wanaume.

Ungependa uhudumiwe na daktari wa jinsi gani katika masuala ya uzazi?

Ni swali ambalo wengi wanaweza kujiuliza, lakini limejaa kwenye mazungumzo ya wanawake, hasa wanapozungumzia hali ilivyokuwa wakati wa ujauzito hadi kujifungua. Katika hali ya kawaida, ungedhani wanawake wanapendelea kuhudumiwa na wataalamu wa masuala ya uzazi ambao ni wa jinsi yao, lakini utakuwa unakosea ukifikiria hivyo; wengi wanapenda kuhudumiwa na madaktari wanaume, Mwananchi limebaini.

Si tu kuhudumiwa wakati wa ujauzito, bali hata wakati wanapotaka kujifungua wangependa wanaume wafanye kazi hiyo.

Lakini hawapendelei wanaume hao kuwapima njia ya uzazi kwa kuingiza mikono. “Napenda sana kuzalishwa na daktari wa kiume kwa sababu wana huruma,” alisema Tatu Hamisi mkazi wa Tabata, ambaye alikuwa mmoja wa watu waliohojiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.