Ni Wakati Wa Kumwagika Na Kilimanjaro ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ni Wakati Wa Kumwagika Na Kilimanjaro !

Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta shindalo linalojulikana kama "Mwagika Challenge”. Hili ni shindano ambalo linawapatia fursa vijana ya kuonesha vipaji vyao ambapo washindi watapata nafasi ya kuwa katika video mpya ya mastaa wakubwa wa Bongoflava.

Shindano hili limeungwa mkono na mastaa kama Shettah na Shilole ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhimiza mashabiki kushiriki shindano hili.

Mshiriki anachotakiwa kufanya ni kuimba Mwagika Tune kwa kuonesha flow yake tu maarufu kama “Song Cover”. Shindano hili linaendelea hadi mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwisho wa washiriki kutuma video zao ni tarehe 30 Septemba 2016.
Washindi 6 wa awali watapata nafasi ya kuingia fainali na baadae watapigiwa kura na mashabiki ili kupata washindi ambao watashiriki katika video rasmi ya muziki ya Kilimanjaro Lager pamoja na mastaa wa muziki Tanzania.

Jinsi ya Kushiriki #MwagikaChallenge

1.      Mshiriki lazima awe na umri wa miaka 18 na kuendelea
2.      Ingia www. http://kililager.com/mwagika kupakua Mwagika Tune
3.      Rekodi video yako ukiimba Mwagika Tune Bongoflava
4.      Tupia video yako kwenye mtandao wa Instagram ukitumia #MwagikaChallenge kisha tag @kili_lager

Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Kilimanjaro Premium Lager kujua zaidi kuhusu #MwagikaChallenge.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.