Mrembo Lupita Nyong’o Aonyesha Kipaji Chake Cha Ku-Rap, Ni Balaa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mrembo Lupita Nyong’o Aonyesha Kipaji Chake Cha Ku-Rap, Ni Balaa !

Umeshawahi kufikiria itakuwaje siku Lupita Nyong’o akaamua kubadili upepo na kuingia kwenye muziki hasa akiwa anarap? Nicki Minaj lazima atafute kichaka cha kujificha.

Kwa wale wasiojua malkia huyu wa filamu ya 12 Years A Slave anaweza pia kurap na hutakiwi kushangaa siku ukisikia amehamia upande wa pili kama wanavyofanya mastaa wengine duniani huku wakiwa wanaimba lakini kwa upande mwingine ni waigizaji pia kama ilivyo kwa kina Kevin Hart, Jamie Foxx na wengine wengi.

Katika kusherehekea kufikisha followers milioni tatu kwenye mtandao wake wa Instagram, Lupita amepost kipande cha video kwenye mtandao huo akionyesha jinsi alivyomkali kwenye kufreestyle.
Hii si mara ya kwanza kwa mrembo huyo akionekana akifreestyle kwa hata wiki chache zilizopita alifanya kama hivyo kwenye kipindi cha ET.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.