Kanye West Ameipiku Rekodi ya Papa Francis ya Mauzo ya Bidhaa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kanye West Ameipiku Rekodi ya Papa Francis ya Mauzo ya Bidhaa.

Stress alizokuwa nazo Kanye West kwenye uwekezaji wake kwenye mambo ya fashion zimeondoka rasmi.
Ni kwasababu kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, rapper huyo mropokaji, ameingiza $780,000 kwa usiku wa Jumatatu pekee kwa mauzo ya bidhaa zake za nguo kwenye ukumbi wa Madison Square Garden.
Mauzo hayo yamevunja rekodi ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ambaye mwaka jana aliingiza $540,000 kwa mauzo ya bidhaa za waumini kama vile rozali, misalaba na vingine kwenye ukumbi huo maarufu jijini New York.

Kanye alikuwa akitumbuiza kwenye ziara yake huku pia akiuza nguo na vitu vingine anavyotengeneza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.