Joh Makini Arekodi Ngoma Mpya na YCEE Kutoka Nigeria. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Joh Makini Arekodi Ngoma Mpya na YCEE Kutoka Nigeria.

Rapper Joh Makini amefanikiwa kuingia studio Jumatano hii kurekodi wimbo na msanii wa Nigeria, Ycee aliyekuwa nchini kwa ziara yake ya siku tatu.

Wawili hao walikutana na kurekodi wimbo huo kwenye studio za Wanene Entertainment wakiwa na Luffa ambaye ameutayarisha wimbo huo.

“#aboutlastnight with @iam_ycee #waneneentertainment studio #WEUSI_X_YCEE #LETSGETBACKTOTHEMUSIC,” ameandika Joh Makini kwenye picha aliyoweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na staa huyo wa Omo Alhaji.
Ycee baada ya kurekodi wimbo na The Amazing

YCEE aliondoka jana nchini kwenda Afrika Kusini huku akiwa tayari ameshafanya wimbo mwingine na kundi la Amazing linaloundwa na Izzo Buzness pamoja na Abela Music.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.