Hilary Clinton Augua Homa ya Mapafu Katika Kumbukumbu ya Wahanga wa Septemba 11. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hilary Clinton Augua Homa ya Mapafu Katika Kumbukumbu ya Wahanga wa Septemba 11.

Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari.

Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amekutwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.
Akijerea baada ya kupata nafuu

Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Donald Trump alihudhuria hafla hiyo.

Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.

Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.