Chris Brown na Wizkid Kutumbuiza Mombasa, Oktoba 8 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chris Brown na Wizkid Kutumbuiza Mombasa, Oktoba 8

Chris Brown na Wizkid wanatarajiwa kutumbuiza pamoja kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival nchini Kenya, Oktoba 8, mwaka huu.

Hiyo itakuwa si mara ya kwanza kwa wasanii hao kutumbuiza pamoja kwani mwezi Juni, mwaka huu walitumbuiza pamoja kwenye show ya ziara ya One Hell of a Nite Tour 2016 ya Chris Brown huko Uingereza na Amsterdam.
Mwaka huu umekuwa ni wa mafanikio kwenye muziki wa Wizkid kutokana na kuonekana kuwa karibu na mastaa wakubwa duniani huku akishirikishwa kwenye nyimbo zao akiwemo Drake, Justine Skye, Chris Brown, Tenie Tempah na Swizz Beatz.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.