Chidi Benz Akanusha Kurudia Kutumia Unga. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chidi Benz Akanusha Kurudia Kutumia Unga.

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amekanusha taarifa ambazo zimezagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amerudia katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Rapper huyo amedai taarifa hizo zinasambazwa na wabaya wake ambao hawamtakii mema.

“Watu wananipenda kuliko kawaida, hata hayo maneno sijui nimerudia kwenye madawa ya kulevya yaani hata hawajali kabisa ila maadui zangu ndiyo wanajali maneno ila watu wangu hata nikitoka sina nguo wao wanaona mimi nimevaa nguo na watabisha hivyo yaani, hayo maneno wanayosema karudia nawaambia kuwa nirudie nisirudie, nifanye nisifanye sijali, mimi nafanya kazi ambayo wananchi walinijua kupitia kazi hii hivyo siwezi kuharibu hata kidogo, nitumie nisitumie sitakosea kufanya ile kitu wananchi walinijua nikifanya” Chid Benz alikiambia kipindi cha kipindi cha Planet Bongo.

Rapper huyo kipindi cha nyuma alikuwa akitumia madawa ya kulevya na baadaye alipelekwa rehabu kwa ajili ya kuacha matumizi ya madawa hayo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.