Argentina Kuivaa Venezuela Bila Messi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Argentina Kuivaa Venezuela Bila Messi

Na Halidi Abdulrahman
Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi ataukosa mchezo unaofuata wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya timu yake dhidi ya Venezuela kutokana na maumivu.

Messi ambaye alitangaza kustaafu kuichezea timu yake hiyo ya taifa, alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Uruguay kwenye ushindi walioupata Argentina wa bao 1-0.

Kocha wa Argentina, Edurgado Bauza amethibitisha juu ya kuumia kwa Messi na kusema kwamba hatamjumuisha kwenye kikosi cha Argentina dhidi ya Venezuela.

"Messi ni majeruhi na hataweza kucheza mchezo unaofuata, hatuwezi kumuweka katika hatari zaidi, tumeongea nae, tumeongea na daktari wake, na inashauriwa kumuacha. Kesho atakuwepo kundini lakini hatakuwa sehemu ya mchezo" alisema Bauza.

Messi atatakiwa kurejea katika hali yake ya utimamu kabla ya Septemba 10 ili kuisaidia timu yake ya Barcelona kwenye mchezo wa Ligi ya Hispania, LaLiga dhidi ya Derpotivo Alaves.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.