Young Killer: Namkubali Dogo Janja Zaidi Kuliko Young Dee Kwasababu Hii Hapa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Young Killer: Namkubali Dogo Janja Zaidi Kuliko Young Dee Kwasababu Hii Hapa.

Star wa Hip Hop anayeuwakilisha mkoa wa Mwanza, Young Killer Msodoki, ameweka wazi kuwa kati ya marapa wenzie wenye umri mdogo Bongo, Dogo Janja na Young Dee anamkubali na kumuelewa zaidi Janjaro.

Young Killer ameweka wazi sababu za kumuelewa Dogo janja, kuwa alimuhamasisha kwamba inawezekana kutoboa na kufanya vizuri kwenye tasnia ya Muziki hata ukiwa na umri mdogo.

Akiongea na Times fm, killer Amedai kuwa kabla ya kumsikia Dogo Janja akivuma, alikuwa akiamini ili ufanye vizuri kwenye muziki lazima uwe na umri mkubwa zaidi. “Unajua nisiwe muongo Dogo janja kanihamasisha sana kupambana nilikuwa naogopa kujaribu, sasa siku ile nipo nyumbani ye ndo anatamba nikasema lazima nimsikilize, hazikupita dakika nyingi nikamsikia redioni nikasema kumbe inawezekana, Young Dee nae ni mkali sana ila mimi namkubali zaidi Dogo Janja.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.