Wolper Aanika Utajiri wa Nyumbani Kwake, Lazima Ushangae Kufahamu Hii. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wolper Aanika Utajiri wa Nyumbani Kwake, Lazima Ushangae Kufahamu Hii.

Staa katika tasnia ya filamu nchini, Jacqueline Wolper, amewaacha Watanzania midomo wazi baada ya kuanika utajiri wa nyumbani kwake kutokana na vitu vya gharama alivyo navyo huku bado akiwa kwenye nyumba ya kupangisha.

Akipiga story kwenye show ya Ujenzi EATV kila Jumapili, Jacqueline Wolper amesema kuwa anapenda kukaa sehemu nzuri nandio maana amenunua vitu vya kupendeza akiwa kwake.

Staa huyu ambaye kwasasa anajimwaga na mwanamuziki wa Bongo flava kutoka WCB, harmonize, Jacqueline Wolper amesema “Sio vizuri kutaja taja bei lakini mfano kama kochi ni milioni 11, meza ni milioni 3 kasoro, kaunta ni milioni 6 kasoro, friji ni milioni 4.6, ile ya vyombo ni kama milioni 3 kasoro, kitanda ni milioni 5 naa hivyo kama milioni 6 kasoro” alijibu swali la gharama ya vitu vilivyopo ndani kwake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.