Wizkid Kulishambulia Jukwaa la Fiesta Mwanza, Jumamosi Hii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wizkid Kulishambulia Jukwaa la Fiesta Mwanza, Jumamosi Hii

Staa wa muziki kutoka Nigeria, ataungana na wasanii wengine wa Bongo Fleva kulishambulia jukwaa la Fiesta Mwanza, Jumamosi hii.

Clouds FM wamethibitisha kumdondosha staa huyo ambaye hashikiki kwasasa Jumamosi, August 20 kwenye show ya ufunguzi wa tamasha la Fiesta.

“Kituuuuuuu #DealDone kwa mara ya kwanza ndani ya Mwanza #StarBoY wako @wizkidayo utatapata kumshuhudia LIVE juu ya jukwaa la #Fiesta2016 #Imooooo,” wameandika Clouds.

Wizkid mwenye amethibitisha kutumbuiza kwenye tamasha hilo,
Hii itakuwa mara ya pili muimbaji huyo anakuja Tanzania. Mwezi October mwaka jana alitumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.