Video: Wema Sepetu Ammwagia Sifa Diamond Platnumz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Wema Sepetu Ammwagia Sifa Diamond Platnumz

Yapata mwezi sasa tangu macelebrity wawili wenye nguvu kubwa ya ushawishi Tanzania waamue kuzikunjua nafsi zao na kuanza kupeana sapoti ili kuijenga Tanzania moja.

Ni mwanadada Wema Sepetu na msanii Diamond Platnumz ambao kwa muda mrefu walikuwa katika matatizo mazito yaliyo pelekea hadi kutengenezwa team kwa mashabiki zao, kitu ambacho kilikuwa hakimpendezi kila mmoja kati yao kwasababu team hizo ndio zilikuwa chanzo kikuu cha uchochezi wa ugomvi wa wawili hao. Kitu ambacho ilifikia hatua hata Wema Sepetu kushindwa kuimba hata nyimbo za Diamond Platnumz akiwa mbele ya macho ya watu ukizingatia yeye ni shabiki wa msanii huyo.

Lakini sasa mambo ni shwari toka wamalize tofauti zao na mwanadada Wema Sepetu anajimwaga tu na ngoma za Platnumz hata akiwa mbele za watu kwasababu wamekwisha weka wazi kuwa hawana matatizo tena.

Mwanadada Wema Sepetu leo mchana ameamua kummwagia Diamond Platnumz sifa za kutosha katika account yake ya Snapchat baada ya kupost video akiwa anaimba nyimbo za Diamond Platnumz na kuandika“The Kid is Talented…. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni….”

Hakuishia hapo Wema Sepetu akarudia tena kwa msisitizo kwenye video nyingine tena na kuandika “I said it… The Kid is Talented…”

Unaweza kuziangalia kwa picha maneno aliyo yaandika Wema Sepetu hapa chini

Unaweza kuitazama hapa chini video hiyo ikimuonyesha Wema Sepetu akiimba nyimbo hizo na kuandika huko Snapchat.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.