Ujauzito Wa Zari Sasa Upo Wazi, Diamond Aomba Ushauri Jina la Mtoto ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ujauzito Wa Zari Sasa Upo Wazi, Diamond Aomba Ushauri Jina la Mtoto !

Diamond atafuta jina la mtoto wake wa kiume baada ya mapema mwezi huu mkali huyo kuthibitisha ujio wa mtoto wake wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Muimbaji huyo alidai kuwa mwezi Disemba mwaka huu anatarajia kupata mtoto huyo wa kiume, lakini baada ya hapo hatakuwa na mpango wa kuongeza mtoto mwingine.

Kwa sasa Diamond ameonekana kutafakari jina la kumpatia mtoto wake huyo mtarajiwa baada ya kutumia mtandao wa Instagram kumwandikia ujumbe mpenzi wake Zari ampatie jina la mtoto wao huyo.

Looking so sexy, my Beautiful and cute Wife @zarithebosslady !!!… Please tell what would you like me to name my Upcoming Son?…
(Tafadhali niambie Mtoto wangu wa kiume unadhani akija nimwite jina gani…?)

Na sasa mimba ya Zari inaonekana wazi baada ya kushare picha kadhaa kwenye Instagram.
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni ametimiza mwaka mmoja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.