The Game na 50 cent Wamaliza Bifu lao Ndani ya Klabu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

The Game na 50 cent Wamaliza Bifu lao Ndani ya Klabu

Moja ya bifu ambalo lilitengeneza stori nyingi katika ulimwengu wa muziki wa HipHop, hatimaye limefanikiwa kuisha, Rapper The Game na 50 cent wamemaliza tofauti zao katika club ya Ace Of Diamonds strip jijini Los Angels.
The Game na 50 cent ni moja ya wasanii ambao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu tangu mwaka 2005, lakini mambo yakabadilika siku ya Jumatatu tarehe 1 mwaka huu pale The Game alipochukua mike na kusema kuwa hana matatizo tena na 50 cent.
Usiku huo ambao ulikuwa Hosted na 50 cent, The Game hakujali juu ya hilo na kuamua kuwatangazia watu kuwa tofauti zao zimeisha kwa sasa na kusema kwamba vitu vyote vilivyotokea ilikuwa ni miaka 12 iliyopita kwahiyo sasa wapo mwaka 2016 inapaswa kusahahu
“What happened that shit was 12 years ago. Niggas ain’t on that shit…It’s 2016. Ain’t nobody on that old shit.” Alisema The Game.
Mpaka sasa Rapper 50 cent hajazungumzia chochote japo kunapicha zilikuwa zinawaonyesha wakiwa wanaongea pamoja kwenye klabu hiyo.

Kipindi cha Nyuma Rapper The Game alishawahi piga picha ya pamoja na Llyod Banks ambayo ilifanya 50 cent kumjia juu Llyod, moja ya vitu ambavyo aliviongea The Game juu ya picha hiyo alimuhasa 50 kwamba miaka mingi imepita na hatuwezi kuendelea kuwa na bifu kwani tayari wote wanawatoto na wanapaswa kumaliza tofauti zao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.